Mwenyekiti
wa Ngome ya Vijana wa chama cha ACT Wazalendo Abdul Nondo amevunja ukimya na
kuongelea kwa mara ya kwanza tukio la kutekwa na watu wasiokulikana katika stendi
ya mabasi ya mikoani na nchi za nje ya Magufuli Mbezi Loius Jijini Dare s Salaam.
Nondo alitekwa
Novemba 30, 2024 alfajiri katika stendi hiyo wakati akiwasili kutokea mkoani
Kigoma kwa usafiri wa basi la Saratoga lenye namba za usajili T 221 DKB na
kuchukuliwa na gari lenye usajili namba T 249 CMV aina ya Landcruise rangi
nyeupe.
Akiongea kwa
uchungu akiwa hospitali ya Aga Khan ambayo amelazwa akipatiwa matibabu, Nondo
amesema alijikuta akizingira na watu wapatao sita alipotoka tu nje ya kituo
hicho na wakamuambia yupo chini ya ulinzi, akae kimya asipige kelele.
“Watu hao
walinizingira na mwanzo nilidhani kuwa ni vibaka walipoanza kunikamata kwa
nguvu nilipiga kelele kuomba msaada kwa watu lakini hakuna aliyekuja kunisaidia
mara nikaona gari nyeupe ikija na kunipakia,” alisema Nondo.
Amesema
akiwa kwenye gari watu hao waliulizana kuwa pingu zipo wapi na walipozikosa
walimfunga kwa kamba mikono yake kwa nyumba na kisha kumfunga kitambaa machoni
asione na kuondoka naye.
Amesema
lifikapahali akashushwa kwenye jengo na kisha kuanza kupigwa na marungu kwenye
magoti, kwenye nyao na kwenye mabega, huku wakimuambi kuwa yeye anajifanya kuwa chamdomo hivyo leo watamuua.
“Baada ya
kipigo hicho zililetwa pingu nikafungwa na kisha miguu yangu ikaingizwa bomba
kati kati nikaning’inizwa kichwa chini miguu juu na kuendelea kuteswa kwa
kupatiwa kipigo,” alisema Nondo.
“Nikiwa
katika eneo hilo nilikuwa nasikia watu kama wakizungumza milio ya magari
ikipita pamoja na ving’ora vya Ambulance (gari la wagonjwa) hali iliyonifanya
kujua kuwa nilipo sipo mbali na barabara,” alisema Nondo.
Amesema
kwamba watekaji hao walibadilisha gari na kumchukua hadi eneo la fukwe ya Coco,
ambayo alikuja kulitambua baadae baada ya kufunguliwa kitambaa na mikondo iliyofungwa
na kutelekezwa.
Amesema
kwamba watekaji hao walimueleza aende nyumbani moja kwa moja na asiongee na
vyombo vya habari la sivyo watakuja kumteka mahala popote atakapokuwapo na
safari hii hawatomuachia hai watamuua.
0 Maoni