Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa Prof. Ibrahim Lipumba ametetea kwa mara nyingine tena nafasi ya uenyekiti baada ya kuibuka mshindi katika Uchaguzi Mkuu wa chama hicho kwa kupata kura 216 kati ya kura halali 592 zilizopigwa huku anayemfuatia Hamad Masoud akiambulia kura 181.
Uchaguzi huo ulikuwa na wagombea 9 akiwemo Ali Juma
Khamis ambaye alijitoa dakika za mwisho, mgombea wa pili ni Athman Kanali
aliyepata kura 5, Hamadi Hamadi kura 181, Juma Shaban kura 6, Maftaha Abdallah
Nachuma kura 102, Wilfred Lwakatare kura 78, Ngaitile Siwale kura mbili na Chifu
Lutalosa Yemba kura mbili.
Wakati wa kutangaza matokeo Mwenyekiti wa Kamati ya
Uchaguzi CUF Taifa amesema “Kwa matokeo haya niliyonayo na kwa nafasi yangu ya
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi namtangaza Prof. Ibrahim Lipumba kuwa ndiye
Mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa uchaguzi wa CUF, ndugu zangu kwa mgombea
ambaye hajaridhika na matokeo tunayo Kamati ya Rufani anakaribishwa kuwasilisha
rufaa yake kwa kamati hiyo.”
Prof. Lipumba amekuwa Mwenyekiti wa CUF kwa miaka 25 sasa
tangu aliposhika nafasi hiyo mwaka 1999.

0 Maoni