Nabii
maarufu nchini Uganda na Duniani Prophet Elvis Mbonye, ametabiria mambo mema
Rais SSH, kwamba utawala na mamlaka yake yatazidi kushamiri na kupanuka mpaka
nje ya Tanzania.
Amesema hayo
leo Jijini Dar es Salaam, katika mkutano wake na viongozi mbalimbali wa
makanisa pamoja na serikali uliofanyika ukumbi The Dome, Masaki.
Amesema
aliamua kuja Tanzania, ili kukutana makuhani wa Mungu, ili awape ujumbe ambao
Bwana Mungu amempa mahsusi kwa ajili ya nchi ya Tanzania.
"Bwana Mungu amenimbia kwamba nchi ya
Tanzania inaenda kungara sana,na itang'ara chini ya Uongozi wa Rais huyu
mliyenaye.Siyo hivyo tu, lakini pia uongozi wa Rais huyu utaenda kukua na
kushamiri mpaka nje ya hapa kwenu.Yatunzeni vizuri haya maneno niyasemayo leo hii."
Miongoni mwa
viongozi wa serikali waliohudhuria mkutano huo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Albert Chalamila.
Katika
salamu zake kwa niaba ya serikali, Bw Chalamila amesema uhusiano wa Uganda na
Tanzania una historia ndefu na hakuna mtu yeyote atayeweza kuuharibu.
"Nakumbuka
nilipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera tulikuwa tuna mikutano ya mara kwa mara ya
ujirani mwema, tukijadili mambo nuhimu ya kuziendeleza nchi zetu hasa kule
pembezoni mipakani.Uhusiano huo utazidi kuendelea maana sisi ni ndugu," amesema.
Kwa mujibu
ya video zake ilizoko Youtube, Nabii huyu amewahi kutabiri mambo mbalimbali,
likiwemo la kuondolewa wa Waziri Mkuu wa Uingereza Rish Sunak, ambapo alitoa
utabiri huo miezi mitano kabla Waziri Mkuu huyo hajajiondoa madarakani.
Aidha,
alitabiri kurejea tena madarakani kwa Rais Donald Trump wa Marekani, jambo
ambalo alilifanya mwaka mmoja na nusu kabla ya uchaguzi wa Marekani uliofanyika
mwaka huu.
Aliwahi pia
kutabiri kutokea kwa mafuriko ya nchini Dubai, jambo ambalo alilifanya miezi
mingi kabla tukio hilo halijatokea.Jambo hilo kweli lilikuja kutokea mwaka huu.
Nabii Mbonye
alitabiri pia mafuriko ya kaskazini mwa Kenya miezi mitano kabla hayajatokea.Na
lilipokuja kutokea lilisababisha maafa makubwa nchini humo.
Aidha, Nabii
huyo pia aliwahi kutabiri kwamba ndege mbili za Uganda zingeanguka nchini
Somalia.Baada ya utabiri huo aliijulisha Serikali ili wasipeleke ndege huko
Somalia.Hata hivyo serikali ya Uganda walimpuuza, na kweli ndege hizo
zilipokwenda huko ilikuja kutokea kweli kama alivyotabiri maana ziliangushwa.
Nabii Mbonye
ana mvuto mkubwa kwa watu wa rika zote nchini Uganda,lakini zaidi zaidi vijana
ambao wanakwenda kwake ili kutatuliwa matatizo yao ya kiroho na kimwili.
Mkutano wake
wa Dar es Salaam uliandaliwa na Umoja wa Makanisa ya Mitume na Manabii
Tanzania, chini ya uongozi wa Rais wa Makanisa hayo Nabii Joshua.
Gharama zote
za maandalizi za mkutano huo zikiwemo za ukumbi, kifungua kinywa na nyinginezo
zimegharimiwa na Nabii huyo wa Uganda ambaye pia ana ukwasi mwingi.
0 Maoni