Mwekezaji kiwanda cha KEDA Tanzania Ceramic Company Limited kimetekeleza ujenzi wa mradi wa ujenzi wa daraja katika Mto Msorwa uliopo barabara ya Mbezi Msorwa Shungubweni Boza yenye urefu wa mita 6 upana mita 7 kina mita 1.5 eneo la Mto Msorwa barabara inayoungansiha kata ya Mbezi na Shungubweni mradi unaotokana na fedha za kurudisha fadhila kwa jamii katika kuunga mkono jitihada za Rais Samia katika kusaidia wananchi kwenye maeneo yenye uwekezaji ili nao wanufaike.
Akizungumza
katika eneo la mradi huo Afisa Biashara Kiwanda cha KEDA Bw. Masoud Suleyman
amesema mradi huo wa kuimarisha miundombinu ya barabara utawezesha kata ya
Mbezi Shungubweni kurahisisha shughuli za kiuchumi na huduma za kijamii kwa wananchi
wa kata hizo na kurahisisha usafirishaji wa malighafi ya mchanga katika
utengenezaji wa bidhaa ya kioo.
"Gharama
za mradi umetekelezwa kwenye kutumia fedha za ufadhili wa kiwanda cha KEDA Ceramics
Tanzania Companya Limited kwa mwaka 2024 gharama ya mradi ikiwa ni shilingi milioni 150 ambapo utekelezaji wake mradi huo umejengwa
kwa kutumia wataalamu,vifaa na malighafi za kiwanda cha KEDA," amesema Sulyman na kuongeza kuwa,
"Utekelezaji
wake umeanza tangu tarehe 28/10/2024 kwa kushirikiana na wataaalamu kutoka
ofisi ya Meneja Tarura Wilaya ya Mkuranga vifaa na malighafi za kiwanda
vimetolewa na kiwanda cha KEDA, manufaa ya mradi utawezesha wananchi kupita
kiurahisi kipindo chote cha mwaka kama misimu ilivyo ikiwemo kipindi cha mvua."
Kwa upande
wao baadhi ya wananchi katika vijiji tofauti vilivyonufaika na mradi huo akiwamo
Mohammed Msumi mkazi wa kitongoji cha kikopi kijiji cha Msolwa anasema walikuwa
wakipata tabu kuvuka katika eneo hilo haswa katika kipindi cha mvua.
"Vijana
walikuwa wakivusha watu kwa pesa lakini KEDA wameona tatizo wamelipanua daraja hili
katika ubora mzuri tunawakaribisha wawekezaji wengine watusaidie ujenzi wa
barababara na daraja tunawashukuru sana wawekezaji kwa ukarimu wao," alisema.
Naye Amina
Mohammed Juma waliwashukuru wawekezaji wa KEDA kwa kuwajengea daraja ambalo
lilikuwa korofi wakati wa mvua eneo
hujaa maji na wananchi magari kukwama kwa kushindwa kupita hali iliwanyima
usingizi wananchi wanaotumia barabara hiyo kwa muda mrefu na kuchangia
maendeleo yao kurudi nyumba.
Nao baadhi
ya viongozi wateule wa serikali za vijiji kikiwemo Msolwa lilipo daraja hilo, Jumanne Mtambwe ni Mwenyekiti Mteule kijiji
cha Kisayani Mkuranga amesema
wanafurahia ujenzi huo kwa kuwa umewanunganisha kijiji cha Kisayani Msolwa na
Shungubweni amesema ujenzi huo utaleta chachu ya maendeleo kwa kuwa barabara sasa
zitapitika vizuri kwani tatizo la daraja limetatuliwa.
"Tunawashukuru KEDA lakini pia tunawaomba
watujengee barabara ambayo kwa sasa inasumbua kutokana na kasi ya magari
yanayobeba mchanga ambao ni malighafi ya bidhaa ya vioo ambayo inatumika katika
kiwanda chao, tunamuombea pia Rais Samia aendelee kuvutia uwekezaji nchini
kwetu ili fursa zifunguke na wananchi tuwe na maendeleo endelevu kama
walivyofanya KEDA," alisema mtambwe.
0 Maoni