Naibu Waziri
Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amewaasa wahasibu barani Afrika
kuisimamia taaluma yao kikamilifu ili kuendeleza umuhimu na mchango na ukuaji
wa uchumi duniani.
Ameyasema
hayo jana Desemba 04, 2024 wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungaji Mkutano wa Pili wa Jumuiya ya
Wahasibu Wakuu wa Nchi za Afrika (AAAG) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa
cha Mikutano Arusha (AICC).
“Nataka
niwaombe wahasibu mtambue kuwa taaluma yenu ni muhimu hata chochote
kinachotokea katika sehemu zenu za kazi mtalaumiwa, hivyo mzuie hasara
zinazoweza kutokea," amesema Dkt. Biteko.
Amewaasa kusimamia taaluma yao kwa kuzingatia misingi
ya kitaaluma hata kama uamuzi wao unaweza kuwa na gharama“ Isimamieni taaluma
yenu kwa wivu mkubwa na kusema ukweli hata kama mtachukiwa, mahali pa kazi ili
kuwe na ufanisi ni muhimu kuwaheshimu wahasibu ili wakupe matokeo tarajiwa.”
Aidha, Dkt.
Biteko amesema ni muhimu kwa wahasibu hao kujiongezea ujuzi ili kuendana na
mabadiliko ya teknolojia.
Pamoja na
hayo amesema wahasibu wanatakiwa kuwa washauri wazuri wa viongozi wao ili
waweze kufanya sahihi, huku akisema AU inategemea wataalamu hao ili kuisaidia
Afrika kunufaika na rasilimali zake.
“ AU
inawategemea nyie wimbo wa Afrika ni tajiri utabaki kwenye vitabu kama
hatutachukua hatua,” amesema Dkt. Biteko.
Naibu Waziri
wa Fedha, Mhe. Hamad Chande amempongeza Mwenyekiti wa AAAG na Mhasibu Mkuu wa
Serikali ya Tanzania kwa kuandaa mkutano mzuri na kuwataka wahasibu kuwa na
kuzingatia maadili ya kazi yao.
“Afrika tuna
utajiri wa kuwa na watu wenye uwezo mkubwa katika kada hii ya uhasibu na ni
imani yangu kupitia mkutano huu utaleta mabadiliko katika nchi zetu.”
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa Nchi za Afrika ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa
Serikali ya Lesotho, Malehlohonolo Mahase amesema Afrika inabadilika katika
masula ya uhasibu, na kupitia mkutano huo wamepata fursa ya kubadilishana
mawazo na ujuzi.
Amesema AAAG
ni bodi ya Kiafrika inayolenga kwenda sambamba na Umoja wa Afrika huku
ikisimamia nguzo za Umoja huo na kuwa mikataba inayoridhiwa na AU inatekelezwa
pia na AAAG ili kuwa na ukuaji endelevu kwa nchi wanachama na Afrika kwa
ujumla.
“ Kipaumbele
chetu kimekuwa ni wahasibu wanavyoweza kusimamia masula ya uhasibu ikiwemo
hazina za nchi zetu, tumezungumzia kada
ya uhasibu, kuimarisha mifumo yetu fedha na kushughulukia upotevu wa fedha
katika nchi zetu,” amesema Mahase.
Mahase
amewataka Wahasibu Wakuu na Wahasibu Afrika kuendana na mabadiliko ya
teknolojia katika taaluma yao sambamba na kujiongezea ujuzi ili kuwa na ufanisi
katika kazi zao.
Ametaja
umuhimu wa wataalamu hao na kusema kuwa Afrika inawahitaji zaidi wakati huu ili
kukusanya mapato na kuzuia njia zisizo halali za mianya ya fedha.
Akizungumzia
baadhi ya maazio ya mkutako huo “Mkutano huu umeazimia kuwa na matumizi bora ya
rasilimali, kutumia mifumo ya kihasibu inayoshabihiana, kuwa mafunzo ya mara
kwa mara kwa watu wa kada ya uhasibu.”
Amesisitiza
“Kuongeza ushiriki wa wananchi kuhusu bajeti katika utekelezaji na utoaji
taarifa ili kuongeza uwazi sambamba na kuwekeza kwenye masuala ya usalama
mtandaoni.”
Katibu
Mtendaji wa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa Nchi za Afrika, Fredrick Riaga
ameipongeza Tanzania kwa kuhakikisha mkutano huo unafanyika kwa mafanikio
makubwa.
Amewashukuru
Wahasibu Wakuu kutoka nchi mbalimbali walioshiriki akisema ni kiashiria cha
kuimarisha sekta ya uhasibu Afrika ambapo washiriki 800 wametoka Tanzania huku
mkutano wote ukiwa na idadi ya washiriki 1,000.
Amesema
zaidi ya washiriki 1500 wamehudhuria mkutano huo kutoka nchi 26 barani Afrika.
Mhasibu Mkuu
wa Serikali ya Tanzania, Leonard Mkude amewasihi washiriki wa mkutano huo
kufanyia kazi yote waliyojifunza ili kuboresha kazi za uhasibu katika nchi zao.
Mkutano wa
tatu wa AAAG umepangwa kufanyika nchini Ghana, Desemba mwaka 2025.
0 Maoni