Waziri wa
Maji Mhe Jumaa Hamidu Aweso (MB) amewasili Seoul nchini Korea Kusini kwa
mualiko maalumu wa Benki ya Exim ya Korea na mfuko wa mashirikiano ya kiuchumi
wa Korea (EDCF) ambapo anatarajia kukutana na Makamu wa Rais wa Benki hiyo
tarehe 06 Desemba 2024 kujenga mashirikiano zaidi baada ya uwekezaji wa
serikali ya Korea kusini katika miradi ya Maji Taka kwa Majiji ya Dar Es
Salaam, Dodoma na Manispaa ya Iringa.
Waziri Aweso
amepokelewa na mwenyeji wake Mheshimiwa Togolani Edriss Mavura, Balozi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Korea Kusini.
Aidha,
Waziri Aweso akiwa Seoul Korea, ametembelea moja ya makampuni makubwa ya
Teknolojia katika Sekta ya Maji ya nchini Korea ya Green Tech. Inc ambayo
imefunga mfumo wa mita janja (Smart Water Managemant System) katika Manispaa 43
nchini humo pamoja na nchi nyingine,ili kujionea Teknolojia hiyo pamoja na
kuona namna mfumo huo unavyofanya kazi.
Waziri Aweso
amesema Mamlaka ya Maji ya Iringa IRUWASA imepanga kufunga "mfumo janja wa
kusimamia Menejiment ya usambazaji maji" Mjini Iringa (Smart Water
Management System).
Mradi huu
utawezesha kupunguza upotevu wa Maji na kusimamia ubora na msukumo wa maji
katika mfumo wote wa usambazaji kupitia mfumo maalumu wa mawasiliano.
0 Maoni