Naibu Waziri
Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema upotevu wa nishati bado ni
mkubwa, hivyo mikakati ya kukabiliana na upotevu huo ni muhimu ili kujenga
jamii inayotumia nishati kwa ufanisi zaidi.
“Tunahitaji
kukabiliana na suala hili kwa kuzingatia mikakati ya matumizi bora ya nishati
ambayo tutaidhinisha hapa leo, Ninawahakikishia wadau wote kwamba Wizara ya
Nishati na Serikali ya Tanzania ziko tayari kusaidia kufanikisha malengo haya
ya kimkakati,” amesma Dkt. Biteko.
Dkt. Biteko
amayasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kikanda wa Matumizi Bora ya
Nishati unaoendelea PAPU Tower Disemba 4, 2024 Jijini Arusha.
0 Maoni