Mbowe ana saa 48 ngumu za kuamua kuhusu familia

 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amejikuta akiwa katika wakati mkumu wa kuamua kufuata shinikizo la familia yake ama familia ya CHADEMA kufuatia kuibuka kwa wafuasi wake wakimtaka agombee tena nafasi ya uenyekiti.

Wafuasi wa CHADEMA leo wamekusanyika nyumbani kwa mwenyeki wa chama hicho, Freeman Mbowe, Mikocheni jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumshawishi achukue fomu kuwania tena nafasi hiyo.

“Nimekuwa na wakati mgumu na familia yangu. Hakuna kipindi familia yangu imenikalia mguu pande kama kipindi hiki, wananiambia baba inatosha, toka achana na siasa rudi nyumbani uendelee na maisha mengine. Sasa familia yangu nayo ina nguvu katika maisha yangu, lakini vilevile na familia ya Chadema nayo ina nguvu sasa," amesema Mbowe na kuongeza,

“Ninaomba mniachie nimesikia rai yenu nimesikia hisia zenu naheshimu hisia zenu naheshimu hisia za wengine wote ambao wamenifikia nimefikiwa na watu wengi, nawaomba mnipe saa arobaini na nane (kuanzia leo Jumatano) leo ni siku ya Jumatano nipeni Alhamisi, nipeni Ijumaa, Jumamosi nitazungumza neno langu la mwisho na waandishi wa habari."

Amewaeleza wafuasi wake hao kwamba saa tano asubuhi siku ya Jumamosi atazungumza na wahariri na waandishi waandamizi hapo hapo kutoa kauli ya mwisho kuhusu mwenyekiti Mbowe naamua nini.

Chapisha Maoni

0 Maoni