Waziri wa
zamani wa Sheria wa Kenya Martha Karua, yupo nchini Uganda kuongoza timu ya
mawakili wanaomtetea mwanasiasa wa upinzani Dkt. Kizza Besigye na mshirika wake
wa kisiasa, Hajj Obeid Lutale, katika mahakama ya kijeshi mjini Kampala hii leo
Jumatatu.
Dkt. Besigye
na Lutale walitekwa nyara na idara za usalama za Uganda mnamo Novemba 16 wakiwa
jijini Nairobi Kenya, ambapo walikuwa wamesafiri kuhudhuria uzinduzi wa kitabu
na Martha Karua.
Siku nne
baadaye, wawili hao walifikishwa katika mahakama kuu ya kijeshi mjini Kampala,
ambapo walishtakiwa kwa makosa manne yanayohusiana na usalama, kumiliki bastola
mbili na risasi nane kinyume cha sheria.
Wiki
iliyopita siku ya Jumatatu, wakili kiongozi wa Besigye na Meya wa Kampala,
Erias Lukwago, alitangaza kwamba Karua atachukua nafasi yake kama wakili mkuu,
ambapo jana Jumapili, Karua aliwasili Kampala kwa ajili ya kesi hiyo.

0 Maoni