Dkt. Biteko awasili Karimjee kuaga mwili wa Dkt. Ndugulile

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili viwanja vya Karimjee leo Desemba 02, 2024 kuuga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, Marehemu Dkt. Faustine Ndugulile.

Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. Samia Suluhu Hassan ataongoza kuaga mwili wa marehemu Dkt. Faustian Engelbert Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika. 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo Desemba 02, 2024 alipowasili viwanja vya Karimjee kuuga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, Marehemu Dkt. Faustine Ndugulile.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akisalimiana na Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson leo Desemba 02, 2024 alipowasili viwanja vya Karimjee kuuga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, Marehemu Dkt. Faustine Ndugulile.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Desemba 02, 2024 akisaini Kitabu cha Maombolezo kwenye msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, Marehemu Dkt. Faustine Ndugulile,  katika viwanja vya Karimjee.

Chapisha Maoni

0 Maoni