Lissu achukua fomu kuwania uwenyekiti CHADEMA

 

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Tundu Lissu, amefika katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti taifa.

Mwanasiasa huyo amefika katika ofisi hizo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam leo, Jumanne majira ya saa 6:20 akiwa na gari lake aina ya Land Cruiser V8, akiambatana na wasaidizi wake.

Lissu alitangaza rasmi nia ya kuwania nafasi hiyo, Desemba 13, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Chapisha Maoni

0 Maoni