Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)
inautaarifu umma na wadau wake kuwa inatarajia kufanya maboresho ya miundombinu
ya mfumo wake wa usajili kwa njia ya mtandao (ORS), kwa muda wa siku mbili.
Taarifa iliyotolewa na BRELA imesema matengenezo hayo
yanafanyika kuanzia leo Desemba 20, 2024 majira ya saa 12:00 jioni hadi tarehe
23 Desemba 2024 saa 1:30 asubuhi. Wakati wa maboresho hayo baadhi ya nyakati za
kukatika kwa mfumo zinaweza kutokea.
BRELA inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaoweza kujitokeza
kutokana na maboresho hayo, imemalizia taarifa hiyo.


0 Maoni