Kamishna wa Maadili, Jaji (Mst) Sivangilwa Mwangesi
amewakumbusha na kuwataka viongozi wote wa umma wanaotajwa kwa mujibu wa Sheria
ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kuwasilisha tamko la rasilimali na madeni yao
kabla ya Desemba 31, 2024.
Amesema hayo leo katika taarifa yake kwa umma
iliyochapishwa kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa sekretarieti ya maadili
ya umma na kuongeza kuwa, hatua hiyo inalenga kuhakikisha uwazi na uwajibikaji
katika usimamizi wa rasilimali za umma, sambamba na kukuza imani ya wananchi
kwa viongozi wao.
Katika taarifa yake, Kamishna Mwangesi amesisitiza umuhimu
wa kuzingatia masharti ya Ibara ya 132(5)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ya mwaka 1977 na kwamba utekelezaji wa takwa hili ni sehemu muhimu
ya kulinda maadili ya uongozi wa umma.
Tamko la Rasilimali na Madeni linatoa taswira ya uadilifu
wa kiongozi katika utumishi wa umma na linapaswa kuwa halisi na lenye taarifa
sahihi, likijumuisha mali zote pamoja na madeni yanayowahusu moja kwa moja

0 Maoni