Basi
lililokuwa limewabeba wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
waliokuwa wakielekea Kenya limegongana na lori la mizigo maeneo ya Mbande,
Kongwa mkoani Dodoma asubuhi ya leo Desemba 06, 2024.
Wabunge hao
walikuwa wakielekea Kenya kushiriki mashindano ya michezo ya Mabunge ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki.
Majeruhi wa
ajali hiyo wamekimbizwa katika Hospitali ya Uhuru na Hospitali ya Benjamin
Mkapa zote za mkoani Dodoma. Tuataendelea kuwaletea taarifa zaidi.
0 Maoni