Rais wa
Syria Bashar al-Assad na familia yake wamewasili Jijini Moscow, vyombo vya
habari vya serikali ya Urusi vimeripoti, vikinukuu vyanzo vya habari katika Ikulu
ya Kremlin.
Assad ambaye
ameondolewa madarakani, aliondoka jana Damascus kwa ndege bila kujulikana
anaelekea wapi. Inadaiwa yeye na familia yake wamepewa hifadhi Urusi.
Hata hivyo
taarifa hizo kutoka Urusi, hazijathibitishwa na vyombo mbalimbali vya habari
vya kimataifa, ingawa inajulikana kuwa Assad amekuwa mshirika wa karibu na
Urusi.
Na ni silaha
kali za Urusi zilizomsaidia kumuweka Bashar al-Assad madarakani kwa miaka tisa
iliyopita.
Wakati huo
huo, Urusi imeomba mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
ili kujadili hali nchini Syria, kwa mujibu wa mmoja wa wawakilishi wake.
0 Maoni