Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt. Noel Lwoga amezindua rasmi vifurushi vya msimu huu wa sikukuu kwa kuwaalika wananchi na wageni wote kwa ujumla kutumia fursa ya mapumziko ya sikukuu kwa kutembelea vituo vya Makumbusho na Malikale nchini.
Hafla hiyo
imefanyika katika kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Jijini Dar es
Salaam.ambapo amewahimiza watanzania kujenga tabia ya kutembelea maeneo haya
adhimu ya kihistoria na Malikale kwa kuwa kumeandaliwa programu maalum za
kuwapa mafunzo na burudani wazazi na watoto wao kwa bei maalum.
Programu
hizo zinajumuisha kuonja vyakula vya asili, michezo ya jadi, mashindano ya
michezo mbalimbali kwa watoto na vijana na wanajamii kupata fursa ya
kujikumbusha asili zao.
0 Maoni