Watu tisa wamefariki dunia katika ajali ya barabarani
iliyohusisha basi la Ngasere High Class na gari aina ya Toyota Noah
zilizogongana kwenye eneo la Tarakea wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raymond Mwangwala amethibitisha
kutokea kwa ajali hiyo.
Ajali hiyo iliyotokea leo Desemba 26, 2024 majira ya
jioni, imesababisha pia majeruhi mmoja ambaye hali yake imeelezwa kuwa ni
mbaya.
0 Maoni