Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA)
inaendelea kupokea wageni katika Hifadhi zake mbalimbali nchini katika kipindi
hiki cha Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.
Hapa ni ndani ya Hifadhi ya Mpanga/Kipengere iliyopo
katika Mikoa ya Mbeya na Njombe ambapo wageni wametembelea kukonga mioyo yao
kwenye maporomoko ya maji yenye mvuto wa kipekee nchini.
TAWA inawakaribisha wote kutembelea Hifadhi zao, ili
upate kuondoa msongo wa mawazo na kuburudisha moyo wako.Mpanga/Kipengere ni
Maalumu Kwa watu maalumu kama wewe.
Wasiliana nao kwa nambari +255 682 673 761 au +255 676
475 541 wakupe fursa ya kufurahia fahari ya nchi yako.
0 Maoni