Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amezindua kamati ya wataalamu ya uchunguzi wa jengo lililoporomoka katika eneo la Kariakoo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuchunguza chanzo cha tukio hilo pamoja na kufahamu ubora na uimara wa majengo yote yaliyoko Kariakoo.
Waziri Mkuu
Majaliwa amekutana na wajumbe wa kamati hiyo leo jijini Dar es Salaam na
kuwataka wahakikishe wanafanya uchunguzi wa kina, uwazi, haki na kwa kuzingatia
viwango vya kitaaluma.
“Fanyeni
kazi hii kwa weledi, Taifa limewatuma nendeni mkaifanye kazi hii na mlete
matokeo,” amesema Majaliwa huku akiiagiza itekeleze majukumu yake kwa kufuata
sheria, kanuni na maadili ya kazi.
Jumamosi ya Novemba
16, 2024, jengo hilo lililopo Kariakoo jijini Dar es Salaam liliporomoka na
kusababisha vifo vya watu 20 hadi sasa pamoja na majeruhi zaidi ya 86.
0 Maoni