Waziri Mkuu aongoza waombolezaji kuaaga miili ya waliofariki Kariakoo

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza waombolezaji kuaga miili ya watu waliofariki baada ya kudondokewa na jengo katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Novemba 18, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kuongoza waombolezaji kuaga miili ya watu waliofariki baada ya kudondokewa na jengo katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Novemba 18, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waombolezaji wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipozungumza nao kabla ya kuaga miili ya watu waliofariki baada ya kudondokewa na jengo katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Novemba 18, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) wakiwa wamebeba miili ya watu waliofariki baada ya kudondokewa na jengo katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Novemba 18, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua muendelezo wa zoezi la uokoaji katika jengo lililodondoka eneo la Kariakoo Jijini Dar es salaam na amesisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu hadi atakapotolewa mtu wa mwisho aliyekwama kwenye jengo hilo. Novemba 18, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Chapisha Maoni

0 Maoni