Waziri wa
Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe, Mhe.
Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amekinadi Chama cha Mapinduzi (CCM) huku
akiwaomba wananchi kuchagua wagombea wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za
Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024.
Dkt. Chana ameyasema
hayo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Lyamkena, Halmashauri ya Mji
wa Makambako Mkoani Njombe leo Novemba 25, 2024.
Amesema Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani a, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha
za miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani humo katika Wilaya zote za Makambako, Ludewa,
Njombe na Wanging'ombe za ujenzi wa barabara, shule, vituo vya afya n.k.
Akizungumzia
Sekta ya Maliasili na Utalii Mhe. Chana amesema Rais Samia amekuwa kinara
katika kutangaza vivutio vya Tanzania hasa kupitia filamu ya Tanzania The Royal
Tour.



0 Maoni