Mtendaji
Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff
amepata tuzo ya utendaji bora na kuwa miongoni mwa Watendaji Wakuu 100,
akitambuliwa ni kinara katika tuzo hizo kwa mwaka 2024, katika kategoria ya
Mtendaji Mkuu wa mwaka (CEO/MD of the year).
Tuzo hiyo
imetolea usiku wa jana tarehe 24 Novemba, 2024 katika ukumbi wa 'The Super Dome'
Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi
katika hafla hiyo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na
Uwekezaji Zanzibar Mhe. Sharrif Ali Sharrif.
Akizungumza
mara baada ya kupokea tuzo hiyo Mhandisi Seff amewashukuru waandaaji wa tuzo
hizo, Ofisi ya Rais-TAMISEMI pia watumishi wote wa TARURA na wadau wengine kwa
ushirikiano wao katika utendaji wa kazi ambapo imemuwezesha kupata tuzo hiyo.
Tuzo hiyo
inayojulikana kama ‘Top 100 Executive List Awards’ huandaliwa na Kampuni ya
Eastern Star Consulting Group na hii ni mara ya nne kufanyika tangu
kuanzishwa nchini
Na.
Catherine Sungura - Dar es Salaam


0 Maoni