Naibu Waziri
Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza Watanzania kushiriki Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Dkt. Biteko
ametoa rai hiyo leo Novemba 25,2024 akiwa mkoani Geita ambapo amesema uchaguzi
huo ni muhimu hususan kwa ukuzaji wa demokrasia nchini.
“Naomba
Watanzania wote waliojiandikisha kwenye Daftari la Kupiga Kura katika Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa katika maeneo yao wajitokeze kupiga kura kwa ajili ya
kuchagua viongozi wao,” amesema Dkt. Biteko.
Amesisitiza
“Viongozi hawa ndio msingi katika nchi yetu, viongozi hawa ndio wanajua watu
wanaishije, wana shida gani na watafanya nini kutatua shida hizo. Ni muhimu
wote kushiriki kuchagua viongozi tunaowataka,” amesisitiza.
Aidha, Dkt.
Biteko amebainisha kuwa kupiga kura ni haki ya kila Mtanzania mwenye sifa hivyo
watu wote wenye sifa wajitokeze kupiga kura ifikapo Novemba 27, 2024.

0 Maoni