Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) leo Novemba 25, 2024
ametembelea Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Viwanda vya Misitu Mafinga (FWITC-
Mafinga) kilichopo Mkoani Iringa na kupokelewa na Mkuu wa Kituo hicho, Berthan
Paul Odelo.
Mhe. Chana
alikagua karakana ya uzalishaji samani, eneo la mtambo wa kukaushia mbao na
kitalu cha miche.
Chuo cha
FWITC kinatoa Mafunzo ya Ufundi Stadi katika ngazi ya Astashada NTA Level I-III
katika fani za Misitu , Viwanda vya Misitu na Useremala.
0 Maoni