Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya
mazungumzo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Thomas Terstegen jijini
Dar es Salaam leo Novemba 20,2024 .
Miongoni mwa
masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na kuendeleza mashirikiano katika kuboresha
miundombinu ya Hifadhi ya Mwalimu Nyerere ili iweze kufikika vizuri, kuendelea
kusaidia uhifadhi unaopatikana Ruvuma kupitia mradi wa GIZ pamoja na kuunga
mkono juhudi za Serikali za uhifadhi katika kukabiliana na changamoto ya wanyamapori
wakali na waharibifu.
Kikao hicho
kimehudhuriwa na Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),
Eliud Mtailuka, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Glory Mndolwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Makumbusho ya
Taifa (NMT), Dkt Gwakisa Kamatula.


0 Maoni