Diwani wa
Kata ya Gagana wilayani Hanang Mhe. Isaya Mbise ameishukuru Serikali kupitia
Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kazi kubwa ambayo
wameifanya katika kata ya Ganana wilayani humo kwa miradi wa
ujenzi na matengenezo ya barabara
ikiwemo barabara ya lami yenye urefu wa Km. 3.02 ambazo zimewasidia katika usafiri na
usafirishaji.
Mhe. Mbise
amesema kwamba ujenzi wa barabara umeweza kuwasaidia wananchi wa Kata hiyo
pamoja na wilaya kwa ujumla kwani
wananchi wengi ni wakulima na kabla ya lami walikuwa na barabara za vumbi ambapo zinahitaji kufanyiwa maboresho kila
wakati.
"Kufanya
ukarabati wa barabara kila wakati ni gharama kwa Serikali na tunajua kufanya
matengenezo ya barabara nchi nzima ni changamoto, sasa kwa ujenzi wa lami
itatusaidia kwa kipindi kirefu, lakini tuipongeze Serikali kwa kazi kubwa waliotufanyia.”
Hata hivyo
Diwani huyo hakusita kuishukuru Serikali kwa kazi waliyoifanya ya kurejesha
miundombinu katika kata yake pamoja na kata nyingine ambapo ziliathirikiwa
wakati wa maporomoko ya mlima Hanang.
"Kwakweli
tunaishukuru sana Serikali na Rais wetu Dkt. Samia kwa kazi iliyofanyika katika
kata zote zilizoathiriwa, wamejitahidi kuirejesha miundombinu na hata sasa hivi
wananchi wanaendelea na shughuli zao za maendeleo kama kawaida."
Aidha,
amesema wilaya kuwa na barabara nzuri
kama hizo imemrahisisha mwananchi kupeleka mazao kwenye masoko na hivyo
kuwainua kiuchumi.
Aliongeza
kusema kuwa katika miradi hiyo TARURA iliwashirikisha katika kila hatua na hata
hivyo wananchi kupata ajira kupitia miradi hiyo.
"Pia
kabla ya kuanza kwa miradi hii wananchi tulijengewa uelewa na kufahamu miradi
hii ni ya kwetu na hivyo tuna ahadi kuitunza ili idumu kwa muda mrefu," aliongeza
Mhe. Mbise.
Naye,
mwendesha bodaboda wa mji wa Kateshi Bw. Festo Manda amesema wanaishukuru Serikali
kwa ujenzi wa barabara hizo kwani awali tope lilikuwa linawasumbuwa katika
uendeshaji wa vyombo vya moto.
"Wilaya
ya Hanang haijawahi kuwa na barabara ya lami tangu kuanzishwa kwake zaidi ya
barabara kubwa ya Babati-Singida, tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa
kuturahisishia maisha wananchi tunaishukuru kwa maendeleo haya na tuna imani
mji wetu wa Kateshi utakuwa na barabara nyingi za lami.
Pia Bi.
Yasinta Bayo mkazi wa Kata ya Ganana amesema sasa hivi wana barabara za lami
ambazo zinaenda kwenye mitaa mbalimbali tofauti na zamani ambapo mtu akibebwa
na bodaboda ilikuwa ni ugomvi na hata walikuwa wakikataa kuwafuata ila sasa
hivi hata usiku unafuatwa na imewarahishia kwenda vituo vya afya na hospitali
ya wilaya.
Awali,
Meneja wa TARURA Wilaya ya Hanang Mhandisi Paul Mlia amesema katika Wilaya yake
hivi sasa wameweza kujenga barabara za lami na kufikia Km. 3.02 pamoja na
kuweka taa za barabarani 47 ambapo awali mji huo haukuwa na barabara za lami kabisa.
Mhandisi
Mlia ameendelea kusema kuwa TARURA wilayani hapo wanahudumia mtandao wa barabara Km. 1050.5 na
kati ya hizo barabara za changarawe Km.
349.69 na udongo Km. 697.79 na katika kipindi cha miaka mitatu wamefanikiwa
kuongezewa bajeti ya ujenzi na matengenezo ya barabara na kuwezesha Km. 96 za barabara kufunguliwa.
0 Maoni