Idadi ya
vifo vya watu vilivyotokana na kuporomoka kwa jengo la ghorofa eneo la Kariakoo
jijini Dar es Salaam imefikiwa 29, baada ya miili mingine tisa kupatikana,
wakati zoezi la uokoaji likihitimishwa leo.
Msemaji Mkuu
wa Serikali, Thobias Makoba, akizungumza na waandishi wa habari leo akiwa eneo
hilo la jengo lilipoporomoka amesema miili hiyo tisa imepatikana wakati
shughuli ya kuondoa kifusi ikiendelea.
Makoba
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) amesema shughuli ya
uokozi imefikia tamati leo siku ya Jumanne Novemba 26, 2024.
Jengo hilo la
biashara liliporomoka Jumamosi asuhuhi Novemba 16, 2024 na kusababisha vifo vya
watu, majeruhi zaidi ya 80 na uharibifu wa mali zenye thamani ya mamilioni ya
fedha.
0 Maoni