Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha
Mapinduzi Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla akizungumza
na Wanachama pamoja na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni
katika Ukumbi wa Kiramuu Hall, leo NOV 04, 2024.
Amesema kwenye kipindi cha kampeni
hakuna kulala Wana CCM wapambane watafute kura ili kukiwezesha Chama cha
Mapinduzi kushinda kwa kishindo kwani Uchaguzi huu hakuna ile kushinda bila
kupingwa japo kuwa kuna Mitaa ,Vijiji na Vitongoji wenzetu hawajaweka watu.
"Pamoja na kwamba kuna dalili za
wenzentu kutosimamisha wagombea kwenye maeneo mbalimbali itakapotea naomba
niongee na wana CCM wa Kinondoni na Nchi nzima kwamba Uchaguzi huu hauna kupita
bila kupingwa msibweteke kwani mmesikia Chama fulani kimesema kitahakikisha hata
kama CCM ndo wameteuliwa tutawapigia kampeni ya kupigiwa kura ya hapana."
0 Maoni