Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshugulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga amewasili
kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kupokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa
huo Missaille Albino Musa leo Novemba 4, 2024.
Mhe. Nderiananga licha ya kusaini
kitabu cha wageni amefanya mazungumzo na Katibu Tawala huyo kuhusu masuala ya
menejimenti ya maafa pamoja na uwajibikaji na utekelezaji wa shughuli za
Serikali mkoani humo.
Aidha, Mhe. Nderiananga yuko mkoani
Arusha kwa lengo la kuhudhuria Mkutano wa Afya Moja Tanzania unaofanyika katika
Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) ukumbi wa Nyasa mkutano ambao
unafanyika kuanzia leo Novemba 04 hadi Novemba 06.
0 Maoni