Viongozi mbalimbali wajitokeza kuaga mwili wa Mafuru

 

Matukio mbalimbali katika picha kutoka katika Viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es Salaam ambapo mwili wa aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru unaagwa leo Novemba 14, 2024.

Viongozi mbalimbali wa Serikali na Sekta Binafsi, Mabalozi pamoja, na familia ya marehemu tayari wamewasili katika Viwanja vya Karimjee tayari kwa zoezi la kuaga mwili wa marehemu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushiriki katika zoezi hilo.





Chapisha Maoni

0 Maoni