WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa
wawekezaji wakubwa na wadogo kwenye sekta ya madini ili kuhakikisha wanaendesha
shughuli zao kwa tija na kusaidia kukuza uchumi wao na wa Taifa kwa ujumla.
Amesema
lengo ni kuwezesha sekta hiyo inaendelea kuongeza mchango wake katika ukuaji wa
uchumi wa nchi kwa kuhakikisha inachangia zaidi ya asilimia 10 katika pato la
Taifa ifikapo 2025. 
“Hii ni
pamoja na kuendelea kuboresha miundombinu ya umeme, barabara, reli, bandari na
viwanja vya ndege ili kusaidia shughuli za madini kufanyika kwa tija na kwa
gharama nafuu.”
Waziri Mkuu
ameyasema hayo leo (Jumanne, Novemba 19, 2024) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Kimataifa wa Madini na Uwekezaji
Tanzania unaofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius
Nyerere, Dar es Salaam.
Amesema
lengo la mkutano huo ni pamoja na kuvutia wawekezaji kutoka nje ya nchi wenye
rasilimali na teknolojia za kisasa, hivyo utasaidia kuongeza mtaji na
teknolojia mpya, pamoja na kuchochea maendeleo ya uchumi wa nchi. Pia, mkutano
huo unalenga kukuza usimamizi bora wa rasilimali madini kwa manufaa ya Taifa.
Mheshimiwa
Majaliwa amesema kuwa mchango wa sekta ya madini katika pato la Taifa umekuwa
ukiongezeka kutoka asilimia 7.3 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 9.0 mwaka
2023. “Ni matumaini yangu kuwa ifikapo mwaka 2025, Sekta ya Madini itafikia
lengo la mchango wa asilimia 10 kwenye pato la Taifa.”
Aidha,
Waziri Mkuu amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wa dhahabu nchini
kutekeleza takwa la kisheria la kuiuzia dhahabu Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
kupitia viwanda husika ili kuisaidia Serikali kutimiza dhamira yake njema ya
kuwa na akiba ya dhahabu;
Katia hatua
nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua mchango wa wachimbaji wadogo
katika uchumi. Hivyo, Serikali inahakikisha inawawezesha kwa kutoa maeneo ya
uchimbaji, huduma za utafiti na uchorongaji, pamoja na umeme kwenye migodi yao,
ambapo hadi kufikia Septemba 2024, zaidi ya migodi 350 ya wachimbaji wadogo
imeunganishwa na gridi ya Taifa.
Vilevile,
Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali imeanzisha ziara za kimafunzo kwa wachimbaji
wadogo, ikishirikiana na Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania
(FEMATA). Mwaka 2023, wachimbaji 95 walitembelea China kujifunza teknolojia ya
kisasa na kutafuta masoko ya madini yao.
Kwa Upande wake, Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2025/16 makusanyo katika sekta ya madini yalichagia kwenye mfuko mkuu wa Serikali kiasi cha shilingi bilioni 135. “Katika mwaka huu wa fedha 2024/25 kuanzia Julai Mosi, sekta ya madini yalichagia kwenye mfuko mkuu wa Serikali kiasi cha shilingi bilioni na lengo letu ni kufikia shilingi trilioni 1 ifikapo Jalai 2025.”
Aidha,
Mheshimiwa Mavunde amesema kuwa Sekta ya madini imeongeza mchango wake katika
pato la Taifa kutoka asilimia 9.3 hadi asilimia 11.3 hivi sasa.
CHANZO: Ofisi ya Waziri Mkuu

0 Maoni