Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetabiri mvua kubwa kwa siku mbili kuanzia leo Novemba 30 hadi Desemba mosi, katika mikoa 11 kwenye kanda tatu tofauti.
Utabiri huo
wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania umeitaja mikoa itakaokubwa na mvua kuwa ni
mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambayo ni Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe na Rukwa.
Mikoa
mingine ni ya ukanda wa Pwani ya Kusini mwa Bahari ya Hindi ni Lindi na Mtwara,
Kanda ya Kati ya Dodoma na Singida na Kanda ya Kusini mkoa wa Ruvuma na Mkoa wa
Morogoro.
Utabiri huo
wa TMA uliotolewa jana Ijumaa Novemba 29, umeeleza matarajio ya hali mbaya ya
hewa kwa siku tano kuanzia leo Jumamosi Novemba 30 hadi Desemba 3, 2024.
Kwa mujibu
wa utabiri huo Desemba mosi kutakuwa na mvua kwenye maeneo machache ya Nyanda
za juu, Kusini Magharibi mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa na Songwe,
Ukanda wa Pwani ya Kaskazini mwa Bahari ya Hindi.
0 Maoni