Rais wa
Jamhuri ya Sudan Kusini na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),
Mhe. Salva Kiir Mayardit, amewasili nchini Tanzania leo kwa ajili ya kushiriki
katika Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi wa EAC.
Mkutano huu
unafanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Arusha, leo
tarehe 30 Novemba 2024.
Mhe. Rais
Kiir alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA),
alipokelewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Selemani Jafo.
0 Maoni