Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema
marehemu Dkt. Faustine Ndugulile alikuwa kiongozi mwenye nidhamu, rafiki wa
kila mtu na kiongozi aliyeweza kutetea vema maslahi ya Taifa.
Makamu wa
Rais amesema hayo alipofika nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na
Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika Dkt.
Faustine Ndugulile Kigamboni Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuifariji
familia pamoja na waombolezaji wote.
Makamu wa
Rais amewaombea faraja na moyo wa uvumilivu wote walioguswa na msiba huo.
Amewashukuru wote walioshiriki katika kuifariji familia wakati huu wa kipindi
kigumu kwao na kutoa wito kwa Watanzania kuendelea kushirikiana katika nyakati
mbalimbali zinazojitokeza katika jamii ikiwemo za majozi na furaha.
0 Maoni