Timu ya
wavuta kamba ya wanaume ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA)
imeendeleza ubabe katika Mashindano ya Mashirika ya Umma, Makampuni na Taasisi
Binafsi (SHIMMUTA) yanayoendelea Mkoani Tanga baada ya leo Novemba 16, 2024
kuivuta timu shindani ya TPDC kwa mivuto miwili kwa nunge.
Mchezo huo
ulioanza kwa mikiki na tambo za hapa na pale kutoka pande zote mbili huku
mashabiki wa timu hizo wakichagiza kwa ushangiliagi wa hamasa, ulizidi kupamba
moto baada ya filimbi ya mwamuzi kupulizwa kuashiria mchezo kuanza na timu zote
kupimana ubavu Kwa kuvutana Kwa kamba.
Huu ni
ushindi wa tatu mfululizo kwa timu hii ambao licha ya kuiweka pazuri kwenye
msimamo, umeifanya iendelee kuwa tishio kwa timu shindani zinazopangwa kucheza
nayo.
Akizungumza
baada ya mechi Mchezaji wa timu ya wavuta kamba ya TAWA Chamganda Khamis
amesema timu hiyo imejiandaa vyema msimu huu kushinda kila mechi iliyo mbele
yao na itahakikisha inaongeza jitihada ili kuwa mshindi wa Kwanza na kuondoka na
medali ya dhababu.
Wakati huo
huo, Timu ya Pete ya TAWA leo imepoteza mchezo wake dhidi ya ARU Kwa kufungwa magoli 23 Kwa 22 , huu ukiwa ni
mchezo wao wa Kwanza kupoteza tangu waanze mashindano haya.
Pamoja na
kupoteza mchezo huo Timu ya TAWA imeonesha ubora na ushindani mkubwa kwa ARU
kiasi ambacho muda wote ilikuwa ikishangaliwa na wa washabiki mbalimbali
waliojitokeza kutazama mechi hiyo.
0 Maoni