Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua meneja wake wa kampeni Susan Summerall Wiles kuwa Mtendaji Mkuu katika Ikulu ya Marekani (White House).
Trump amesema
katika taarifa yake kwamba Wiles "alinisaidia kufikia ushindi mkubwa zaidi
wa kisiasa katika historia ya Marekani.”
Kulingana na
kambi ya Trump, Wiles atakuwa mwanamke wa kwanza kuhudumu katika nafasi hiyo.
Susie Wiles,
anaelezewa kama mshirika wa kisiasa anayeogopwa zaidi na anayejulikana sana
Marekani na vyombo vya habari nchini humo.

0 Maoni