Naibu Waziri
Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko anaiwakilisha Serikali katika
sherehe za uapisho wa Rais Mteule wa Botswana Gideon Duma Boko zitakazofanyika
Katika Uwanja wa Taifa wa nchi hiyo leo Novemba 8, 2024.
Akiwasili
katika Uwanja wa ndege wa Gaborone, Dkt. Biteko amepokelewa na Katibu Mkuu wa
Vijana, Jinsia, Utamaduni na Michezo, Bridget John, Balozi wa Tanzania Nchini
Afrika Kusini, Mhe. James Bwana pamoja na maafisa wengine waandamizi wa Nchi
hiyo.
Mhe. Gideon
Duma Boko ni Rais wa Sita Botswana kupitia chama cha Umbrella for Democratic
Change.
Uchaguzi
Mkuu nchini Botswana ulihitimishwa tarehe 30 Oktoba, 2024 ambapo Rais Mteule
Gideon Boko aliibuka mshindi katika uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo.


0 Maoni