Mbunge wa
Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ameongelea vipaumbele muhimu
vya kukuza uchumi wa Taifa kwa kiwango cha asilimia kumi (10%)
Akichangia
hoja Bungeni leo jijini Dodoma Prof. Muhonga amesema, “Huko vijijini kwa wakati
huu hii bajeti tunayoitaarisha mwakani maeneo matatu lazima tuyawekee mkazo
sana; nayo ni maji, umeme na barabara.”
“Nadhani bajeti
tutakayoitayarisha mwakani itazingatia hayo, lakini tunamiradi mingi huenda
fedha zisitoshe, napendekeza mbali ya fedha za makusanyo ya TRA tuanze
mazungumzo na mabeki ili tuweze kukopa kwa riba ndogo na pengine tupate fedha
kwenye Stock Exchange (Soko la Hisa).”
Aidha, Prof.
Muhongo, amelieleza bunge kuwa kuna fursa nyingi za ajira nchi za nje ambazo
zinahitaji wageni mabingwa wenye utaalam, na kuongeza kuwa wasiowataka kule ni
hawa wakimbizi.
Amesisitiza
kuwekeza zaidi katika masomo ya Sayansi ili kuzalisha wataalamu wabobezi ambao
sio tu watakazana kutafuta ajira za ndani pekee, bali pia wataweza kuingia
katika soko la ajira za nje.
Ili tutoke
kwenye ukuaji wa uchumi wa asilimia 5-6 kwenda kwenye uchumi wa asilimia 10, mimi
nafikiri ni lazima sasa tuwekeze kwenye maeneo manne, kwanza elimu iandane na
ajira, tuwekeze kwenye uchumi wa hellium na gesi, kwenye kilimo cha biashara
madini na utalii, ameshauri Prof. Muhongo.
Pamoja na
mambo mengine Prof. Sospeter Muhongo, ameishukuru Serikali kwa utekelezaji wa
miradi miwili mikubwa jimboni mwake.
“Mheshimiwa
Rais alipokuwa jimbo la Musoma Vijijini nilimuomba miradi mikubwa miwili barabara
ya Km 92 na kufufua kilimo kikubwa cha umwagiliaji nashukuru kwamba vyote
vimefanikiwa pongeze kwake na pongezi kwa TANROADS,” alisema Prof. Mugongo.
Ameeleza
kuwa barabara hiyo kwa wakati huo ilikuwa na gharama ya dola milioni 150
matangazo yametoka wakandrasi wengi wameshabikia na sasa wapo katika hatua ya
manunuzi.
Prof.
Muhongo ameongeza kuwa barabara hiyo ina daraja ambalo ujenzi wake utagharamiwa
na World Bank (Benki ya Dunia) ambapo lipo katika hatua ya manunuzi, nalo pia
litakamilishwa.
Kuhusu
Kilimo cha Umwagiliaji nashukuru Mhe. Hussein Bashe na Wizara ya Kilimo wanaenda
vizuri hivi karibuni nadhani mwakani tunaanza kujenga miundombinu ya
umwagiliaji,” amesema Prof. Muhongo.

0 Maoni