Jeshi la
Polisi Mkoani Songwe limesema limekamilisha mahojiano na kada wa CHADEMA, Mdude
Nyangali na wamempeleka mkoani Mbeya kwa mahojiano mengine na jeshi hilo kujibu
tuhuma zinazomkabili.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Kamanda wa Polisi mkoani Songwe, Agustino Senga,
amesema tayari wamemaliza mahojiano na mwanaharakati huyo, na tayari ameelekea
Mbeya kujibu tuhuma nyingine zinazomkabili.
Nyagali
alikamatwa Novemba 22, 2024 mkoani Songwe akiwa na makada wengine wa Chadema
akiwamo Mwenyekiti wake Taifa, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Kanda ya Nyansa,
Joseph Mbilinyi 'Sugu' kwa madai ya kukiuka taratibu za kampeni za uchaguzi wa
Serikali za Miraa.
Hata hivyo,
makada wengine waliachiwa na Polisi wakiwamo Mwenyekiti wake Taifa, Freeman
Mbowe, Mwenyekiti wa Kanda ya Nyansa, Joseph Mbilinyi 'Sugu', ila Mdude aliendelea
kushikiliwa kwa ajili ya mahojiano.
0 Maoni