Aliyekuwa
Spika wa Bunge la Wawakilishi la Marekani Bi. Nancy Pelosi amesema Chama cha
Democrats kingeweza kufanya vizuri katika uchaguzi wa rais iwapo Rais Joe Biden
angejitoa mapema kwenye kinyang’anyiro.
Pelosi mmoja
wa wanasiasa wenye nguvu Washington, ameliambia jarida ya New York Times kwamba
“Iwapo rais angejitoa mapema, kungeweza kuwapo na wagombea wengine kwenye mbio
za urais.”
Kauli yake
hiyo imekuwa ya kwanza ya kushutumiana ndani ya chama cha Democrats baada ya
chama hicho kushindwa kuendelea kuwapo Ikulu na kunauwezekano wa kupoteza
nafasi za kwenge Baraza la Congress Jumanne.
0 Maoni