Alexander Isak amefunga goli pekee lililoizamisha Arsenal na kupoteza point tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Newcastle.
Raia huyo wa Uswidi alifunga goli hilo
kwa kichwa baada ya the Gunners kushindwa kuokoa mpira langoni mwao.
Katika mchezo huo uliopingwa dimba la
St James’ Park, Arsenal alianza vizuri, ila Isak alipofunga walishindwa kuwa
wabunifu katika umaliziaji.

0 Maoni