Mkurugenzi Mtendaji wa Dar24 Media na
Mfanyakazi wa Kampuni DataVision International Limited, Maclean Godfrey
Mwaijonga, aliyeripotiwa kupotea Oktoba 31, 2024 baada ya kutoka ofisini kwake
amepatikana.
Akiongea na waandishi wa habari,
Kamanda wa Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne
amesema Mwaijonga amepatikana jana Kigamboni akiwa katika hali ya kutokua na
nguvu ambayo inatokana na kunywa kinywaji kinachosadikika kuwa na kitu
kilichopoteza fahamu zake.
“Jioni ya leo (jana) tumepokea taarifa kutoka
kwa ndugu wa karibu kuwa Mwaijonga ameonekana Kigamboni, tukaongozana na
familia mpaka huko Buyuni na kumkuta akiwa hana nguvu, tukampeleka Hospitali
tunashukuru hana tatizo,” amesema Kamanda Muliro.
Mwaijonga inadaiwa alipotea Oktoba 31, 2024 wakati anatoka ofisini kwake eneo la Rose Garden, Mikocheni jijini Dar es Salaam akiwa na gari yake aina ya Toyota Prado nyeusi yenye usajili namba T 645 DEE.

0 Maoni