Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali
Jacob John Mkunda amewasili nyumbani kwa Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali David
Bugozi Musuguri wilayani Butiama Mkoani Mara tarehe 03 Novemba 2024 kwa ajili
ya kutoa salamu za pole kwa wafiwa na kukagua maandalizi ya Mazishi ya Hayati
Jenerali Musuguri yatakayofanyika tarehe 04 Novemba 2024.
Jenerali Mkunda amesema kuwa
maandalizi yote yamekamilika na kuwashukuru wananchi wa Butiama na maeneo ya
karibu kwa kushiriki katika kutoa heshima za mwisho kwa marehemu ikiwa ni heshima kwa kiongozi huyo aliyetoa
mchango mkubwa katika Ulinzi wa taifa letu.
Jenerali Musuguri aliyefariki dunia tarehe
29 Oktoba 2024 akiwa na umri wa miaka 104 atazikwa nyumbani kwake kwa heshima
zote za kijeshi.



0 Maoni