Chagueni viongozi watakaowatendea haki wananchi- Mbowe

 

Mwenyekiti wa Chama cha Siasa cha CHADEMA Freeman Mbowe amewataka viongozi wa chama hicho watakaochaguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa watende haki kwa wananchi pindi waingiapo madarakani.

Akiwapigia kampeni viongozi wa Chadema Mkoani Mbeya, Mbowe amesema kuwa uchaguzi huu unatoa fursa ya kuwaondoa madarakani viongozi wasiofaa na kuwaingiza madarakani viongozi wanaofaa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu.

"Sisi CHADEMA tunawachagua viongozi wanaotenda haki, na kama endapo kiongozi wa CHADEMA aliyechaguliwa atashindwa kutenda haki kwa wananchi tutamuondoa hatuta subiri mpaka miaka mitano," amesema Mbowe.

Pamoja na mambo mengine Mbowe akiongea katika eneo la Igawiro amewataka wananchi wachague viongozi wa CHADEMA ili wawatumikie wananchi kwa kuzingatia misingi ya chama hicho inayojengwa katika msingi wa haki.


Chapisha Maoni

0 Maoni