Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) imezifungia taasisi fedha 18 zinazotoa huduma ya mikopo
kidigitali kutokana na kutoa huduma hiyo bila ya kuwa na leseni pamoja na
idhini kutoka BoT.
Taarifa
iliyotolewa leo na Gavana wa BoT Emmanuel Tutuba imesema wameyafungia majukwa ya
Programu Tumizi (Application) ya taasisi hizo zilizokiuka mwongozo kwa watoa
huduma ndogo za Fedha Daraja la Pili.
Benki Kuu ya
Tanzania inashirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzifungia
programu hizi ili kuepusha umma kutumia huduma za fedha zisizokuwa na vibali
vya mamlaka husika, imesema taarifa hiyo.



0 Maoni