Jeshi la
Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Juma Afyusisye (38) Dereva Bodaboda, Mkazi
wa Iwambi Jijini Mbeya kwa tuhuma za kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili nwanafunzi
wa kiume wa Darasa la Pili wa Shule ya Msingi Iwambi Mkazi wa Iwambi kwa kumchoma
moto.
Kamanda wa
Polisi Mbeya SACP Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea Novemba 05, 2024
maeneo ya Iwambi Jijini Mbeya, ambapo inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo kutumia
shilingi 10,000/= ya Dereva wa Bodaboda
huyo.
Akisimulia
tukio hilo Kamanda Kuzaga amesema Dereva wa Bodaboda alimpatia mwanafunzi huyo
shilingi 10,000/ na kumuagiza aende dukani kumnunulia maandazi ya shilingi elfu
5,000/= lakini aliitumia pesa yote kwa matumizi yake binafsi.
Baada ya
mwanafunzi huyo kuzitumia fedha hizo alirudi bila pesa na ndipo Dereva Juma
alijichukulia sheria mkononi kwa kummwagia mafuta ya Petroli kwenye shati alilovaa
na kisha kuwasha kiberiti na kumsababishia majera hasehemu mbalimbali za mwili
wake.
Mwanafunzi
huyo amelazwa katika Hospitali Teule ya Ifisi katika Mji Mdogo wa Mbalizi akiendelea
kupatiwa matibabu.
0 Maoni