Shirika la
Reli Tanzania (TRC) limesema kuwa kumetokea ajali ya basi la abiria lililoigonga
treni ya mizigo namba Y611 iliyokuwa ikitokea Kigoma na kusababisha mabehewa 30
kuanguka, ambapo pia katika ajali hiyo abiria 14 wamejeruhiwa hakuna vifo.
Taarifa
iliyotolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano cha TRC, Fredy Mwanjala imesema
kuwa ajali hiyo imetokea usiku wa kumkia leo, ambapo dereva wa basi hilo
alilipita basi lingine lililokuwa limesimama kuipisha treni na kuigonga treni.
0 Maoni