Askari wanajamii 92 kutoka Tanga,
Katavi, Kigoma na Rukwa wamehitimu mafunzo ya kozi fupi katika Taasisi ya
Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi (PWTI).
Mafunzo haya yamewajengea uwezo na
umahiri askari hao wa vijiji vinavyojishughulisha na uvuvi na uendelezaji
misitu. Mafunzo haya yalianza tarehe 22-08-24 hadi 01-11-24.
Mahafali haya ya kozi fupi ilijumuisha
askari wanajamii 42: Village Fisheries Scout (VFS) waliofadhiliwa na Jane
Goodall Institute na askari wanajamii hifadhi za misitu 50: Village Forest
Monitors (VFM) waliofadhiliwa na Shirika la chakula duniani kupitia mradi wa
Fish4ACP-FAO Tanzania.
0 Maoni