Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina na Kampuni ya AMSONS Group ya Uswisi wameingia makubaliano ya kuwekeza dola milioni 300 (zaidi ya shilingi bilioni 800) katika upanuzi wa kiwanda cha Saruji cha Mbeya Cement na kuanzisha kiwanda kipya cha saruji Tanga.
Mbeya Cement, imetangaza kuongeza
uwekezaji kwenye kiwanda hicho kwa kufunga mtambo mkubwa utakaowezea kuzalisha malighafi
(clinker) za kutengeneza saruji tani 5,000 kwa siku kutoka tani 1,000
inazozalishwa sasa.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam
leo Oktoba 15, 2024, na Msajili wa Hazina, Bw. Nehemia Mchechu akiwa pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa Amsons Group, Bw. Edha Nahdi.
Sambamba na uwekezaji huo, Serikali
kwa kushirikiana na mbia huyo, Amsons Group, pia wataanzisha kiwanda kingine
cha saruji mkoani Tanga, kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha malighafi
(clinker) tani 5,000 kwa siku.
“Kwa hiyo maamuzi ambayo sisi kama
wanahisa tumeyafanya ni kwenda kuongeza upanjuzi na kujenga kiwanda kipya na
hivyo kuonegza uzalishaji wetu kutoka tani 1,000 za sasa na kufikia tani 10,000
za clinker kwa siku,” amefafanua Bw. Mchechu.
Naye Mkurugenzi wa Fedha Mbeya Cement,
Bw. Ahmed Mhada, amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutapelekea uzalishaji wa
saruji kufikia tani milioni 4.2 kwa mwaka.
0 Maoni