Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
Mhe. Dkt. Doto Biteko, amesema kuwa Tanzania inayo nafasi kubwa ya kujifunza
Teknolojia ya uwambaji wa magari (Assembling) yanayotumia umeme kutoka kiwanda
cha magari cha HYUNDAI kwani ni rafiki kwa mazingira na hupunguza uchafuzi wa
hali ya hewa.
Dkt. Biteko ameyasema hayo leo Oktoba
23, 2024 nchini Singapore mara baada ya kutembelea kiwanda hicho ikiwa ni ziara
mojawapo kwenye mkutano wa Wiki ya Nishati nchini Singapore na kusema kuwa
Teknolojia kama hizi zina mchango mkubwa kwenye kuinua uchumi wa nchi na
kuongeza pato la Taifa.
‘’Nawapongeza sana wenzetu hasa kwa
Teknolojia na ubunifu wa haya magari pamoja na Teknolojia ya Kilimo janja
(smart farm) ambapo kwanza inatumia nafasi ndogo lakini matokeo yake ni makubwa
sana,’’ alisema Dkt. Biteko.
Kuhusu Teknolojia ya kilimo janja
ambacho kinaendeshwa na kampuni ya ubunifu ya HYUNDAI kwa kutumia Teknolojia
mnemba (Robot) Dkt. Biteko amesema, uwepo wa Teknolojia kama hii unaongeza
tija, inapunguza gharama kwenye uendeshaji wake.
Naye, Makamu wa rais na Mkuu wa
Biashara na mipango kutoka HYUNDAI Motor Group amesema mafanikio hayo
yanayokana na kutumia fursa iliyopo wakati wa changamoto zilizokuwepo awali
kama ya matumizi ya mafuta kwenye magari ambapo haikuwa rafiki kwa mazingira
pamoja na uhaba wa maeneo kwa ajili ya kilimo nchini Singapore.
0 Maoni